25.05.2018: BAADHI YA WATU WALIOKOKA KATIKA IBADA YA KUIOMBEA FAMILIA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

// ZABURi 84:11: Kwa kuwa BWANA, Mungu ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hawatawanyima kitu chema hao waendao kwa ukamilifu. //

Baada ya waongofu wapywa hawa kutambua kuwa "BWANA ni jua na ngao" katika maisha yao, basi siku ya Jumapili 20.05.2018 waliamua kukata shauri na kuokoka katika ibada ya "KUIOMBEA FAMILIA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" jijini Dar es Salaam kwa Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare.

Mch. Elizabert Lucas aliwaongoza sala ya toba baada ya kuhubiri Habari Njema za Mungu katika kipindi cha Sunday School. Waongofu hawa kwa hiari yao waliamua kuinuka katika viti vyao na kwenda madhababu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwaajili ya kuongozwa sala ya toba na kuombewa. Wachungaji wa kanisa hili baada ya waongofu kuongozwa sala ya toba waliweza kuwaombea na kuwatamkia baraka katika maisha yao mapya ya wokovu.
Wakati wa kiombewa baadhi ya waongofu wapya walitokwa na mapepo na nguvu za giza zilizokuwa zikiwatesa kwa muda mrefu.

Baada ya sala ya toba na maombezi, waliweza kubatizwa kwa maji mengi na siku ya Jumatatu na Jumanne ni siku zao za kujifunza masomo ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Masomo yao yanaanza saa 10 jioni.

Tunamshukuru sana Mungu kwa kutoa neema na utukufu kwa waongofu wapya na kuwafanya kiumbe kipya. Na ameahidi kuwa hatawanyima kitu chema hao waenda kwa ukamilifu.
Tunapenda kukushukuru wewe ambaye ulihusika kuwahamasisha hawa ndugu zetu kuokoka. Kazi uliyofanya ni kubwa sana katika kuujenga ufalme wa Mungu. Ni maombi yangu Mungu akafungue milango ya mafanikio ya kimwili na kiroho katika maisha yako. Pia ninakuomba uendelee kuwaleta watu hapa kanisani Mlima wa Moto Mikocheni "B" ili waweze kumrudia Mungu na kuishi amaisha ya kumpendeza Mungu kwa kipindi hiki kifupi cha kuishi hapa duniani.

Yawezekana unatamani kuokoka na kuishi maisha mema ya kumpendeza Mungu, tunakualika katika ibada ya Jumapili hii ambayo itaanza saa 3 asubuhi hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B". Wachungaji watakuongoza sala ya toba, watakuombea na utapata nafasi ya kubatizwa kwa maji siku hiyo hiyo.

Mch. Elizabert Lucas






























































Comments