20.05.2018: BAADHI YA WATU WALIOBATIZWA KATIKA IBADA YA KUIOMBEA FAMILIA

// ZABURI 84:4: Mungu wa wokovu wetu, uturudishe, uikomeshe hasira uliyo nayo juu yetu.//

Hasira ya Mungu ikikupata hautakuwa salama kabisa. Utashangaa mambo yanaanza kuharibika, afya yako inabadilika na kuwa mbaya, unakosa kibali mbele za Mungu na mbele za wanadamu, unaandamwa na mikosi na balaa kwa kila jambo utakalokuwa ukilifanya na mabaya yote yanakuwa upande wako. 

Pengine unaweza kuwa na majumba, magari na mali nyingi lakini huna amani ndani yako, huna furaha ya mali zako, ndugu zako na marafiki zako ndio wanaofaidi mali zako, unakuwa ni mtu wa majuto na mawazo yasiyo na kikomo.

Njia mojawapo ya kuepuka hasira ya BWANA katika maisha yako ni kutubu dhambi zako, kufanyiwa maombi, kufunga na kuomba, kushiriki ibada za kila siku kanisani kwako, kuwaonyesha upendo kwa kila mtu bila kuchagua dini au kabila, kubatizwa kwa maji mengi, kujifunza Neno la Mungu ili kujua ni vitu gani Mungu anatuelekeza ili hasira yake isiwe juu yetu na vizazi vyetu. Unapojua siri za Mungu ndipo milango ya mafanikio inaaza kufunguka katika maisha yako.

Tuna kila sababu ya kumshukuru sana Mungu kwa kuwaokoa watu kutoka katika maisha ya kutompendeza na kuanza maisha mapya ya wokovu. Siku ya Jumapili 20.05.2018 katika ibada ya KUIOMBEA FAMILI iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" watu wengi waliweza kuokoka na kubatizwa kwa maji mengi. Katika ibada hii watu wengi sana walijitokeza katika madhabahu ya Mungu na kuamua kuokoka. 

Mch. Elizabert Lucas aliweza kuwaongoza sala ya toba na baade wachungaji wa kanisa hili waliweza kuwaombea na kuwatamkia baraka waongofu wapya. Baada ya maombezi waliweza kubatizwa kwa maji mengi na kujazwa Roho Mtakatifu. BWANA aliwasamehe dhambi zako na kuwafanya viumbe vipya.

Siku ya Jumatatu na Jumanne ni siku maalum kwa waongofu wapya kuanza masomo ya kukulia wokovu ambayo yanatolewa katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare. Masomo yanaanzia saa 9 alasiri.

Kama Yesu alibatizwa kwa maji mengi iweje wewe usibatizwe maji mengi?. Kwahiyo kubatizwa kwa Mkristo ni kitu muhimu sana, na kama hujabatizwa tunakualika katika ibada ya Jumapili hii kutakuwa na ubatizo kwaajili yako. Njoo na rafiki au ndugu zako ili nao wababtizwe kwaajili ya kuanza maisha mapya ya kumpendeza Mungu.

Unapobatizwa unapata amani ndani katika maisha yako, unapokea Roho Mtakatifu, unakuwa na hofu ya Mungu, maisha yako yabadilika na kuwa bora zaidi, unaongozwa na Mungu kwa kila jambo unalotaka kulifanya, Roho Mtakatifu anakuongoza katika njia zako, uanapata upendeleoa kutoka kwa Mungu na maisha yako yanafanikiwa kimwili na kiroho.

Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3




































































Comments