13.05.2018: WATALAAMU WA MITANDAO-SADAKA NETWAORK WATEMBELEA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Watalamu wa huduma ya Mungu kwa njia ya mitandao kupitia tovuti yao ya SADAKANETEWORK.COM kutoka Israel waliweza kufika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na kuweza kuwasalimu waumini wa kanisa hilo na pia kuelezea umuhimu wa tovuti yao ya SADAKANETWORK.COM. Kwa Tanzania watumishi wa Mungu wakubwa wameweza kujiunga na tovuti hiyo na sasa wananfurahi matunda yake.

Unaweza kuingia sasa www.sadakanetwork.com utajionea mambo yanaoendelea huko. Mungu akubariki sana kwa kulipenda kanisa lako la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na ninaamini kupitia Sadaka Network unaweza kubarikiwa na kusapoti huduma yako ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" ili isonge mbele kwaajili ya kazi moja tu ya kuwaleta watu kwa Yesu na kuokoa roho za watu zinazoteseka na magonjwa na shida mbalimbali.

Tukualike katika ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3.







Comments