13.05.2018: MHE BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE SIKU YA JUMAPILI YA MOTHER'S DAY ALIA NA WATU WASIOWAJALI MAMA ZAO

Katika ibada ya UKOMBOZI WA MWANAMKE iliyofanyika siku ya Jumapili ya Mother's Day 13.05.2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kuhubiri ya KUMTHAMINI MAMA na hivi ndivyo alivyohubiri:-
Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare



MAMA YAKO NI DAKTARI ASIYESOMEA UDAKTARI...
Katika siku ya Mother’s Day 13.05.2018 tungependa kuwashukuru rasmi akina mama kwa kazi nzuri mnazofanya. Mama ni daktari asiyesomea udaktari, hana cheti cha udaktari wala diploma wala “degree” lakini ni daktari wa ajabu ndani ya nyumba au familia. Leo ni siku tunayoshangilia kwa kazi nzuri wanazofanya akina mama. amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha unakuwa na afya njema, ulipoumwa amehangaika kukutafutia matibabu. Ukiungua tu amekuwa wa kwanza kukupata “Firts Aid” kabla ya kwenda hospitalini. Mpe haki yake mama siku ya leo. Mtafutie zawadi nzuri



MAMA YAKO MPE HAKI YAKE. KACHANGIA MAFANIKIO YAKO
Mwanamke amepewa kipaumbele na kutahamniwa sana. Mara nyingi tumekuwa sikuku ya wanawake ya tarehe 3.8 kila mwaka na tunakuwa na siku ya Mother’s day. Na sisi wana Mlima wa Moto Mikocheni “B” kama kanisa tunaungana na ulimwengu kuwashangilia akina mama kwa kazi nzuri ambazo wamekuwa wakizifanya mwaka hadi mwaka; “Wakina mama Hongereni sana”. Tukitafakari kazi za akina mama ni nyingi sana, lakini wameshirikiana na Mungu kuleta viumbe duniani na ndio maana kila mwanamke au mwanaume anayetembea barabarani ana mama yake, ila asingekuwepo mama hatungewaona wakipita barabarani.



KAZI ALIZOFANYA MAMA JUU YAKO HAZIHESABIKI 
Akina mama wamefanya kazi kubwa na nzito sana kuhakikisha na wamejinyima starehe zao ili sisi tunaendelea kuishi kwaajili ya maisha yetu hapa duniani. . Sufuria walizoosha akina mama kama zikipangwa basi zinaweza kufika hata Nairobi Kenya, vyakula walivyopika akina mama ukivipanga vinaweza kufika hata Kampala Uganda, akina mama wamekuwa dobi wa kufua “Jeans”, suruali, mashati ya waume zao na watoto wao bila kulipwa. Tangia wameanza kufua nguo wakizianika zinafika Zanzibar. Ni zamu yako ya kumthamini mama yako, kumpa furaha, kumpa raha, kumfariji ili naye ajisikie wakati bado anaishi duniani na sio akifa ndio uanze kutoa maua.



KWANINI UMTUPE MAMA YAKO ALIYETESEKA KWAAJILI YAKO?
Ni nani kama mama? Wamama ni madaktari wa kwanza, pale mtoto anapolia kwa ugonjwa. Mtoto akiumwa wao wameshagundua kitu kinachomsumbua na kutoa “solution”, basi wanamchukua mtoto na kumuweka kifuani, mama anamlaza mtoto kwenye “nyonyo” na kama ana homa “anamsisponji” mpaka homa ishuke na baadae anampeleka hospitalini kwa daktari kwaajili ya matibabu kamili. Kwahiyo mama anahitaji pongezi, kuthaminiwa, kuheshimiwa, kutunzwa kwasababu amefanya kazi kubwa sana katika maisha yako. Leo hii unalinga mitaani, una gari una kila kitu kwasababu ya mama. Naomba umwambie mama yako; “Hongera mama, asante mama”. Usimtupe mama.



KWANINI UMEKOSA SHUKRANI KWA YALE ALiYOFANYA MAMA YAKO?
Kuna watu hawana shukrani kwa mama zao kwa mema waliotendewa. Na ndio maana imetengwa Mother’s Day ili kumwambia mama yako “Asante”. Mama halipwi mshahara kwa kila kazi anayofanya lakini hakuna mtu anayempa shukrani. Baadhi ya baba wanawakalipia mama zao wanapopikiwa chakula, wanasema kwa ukali eti “Wee! mama umezidisha chumvi kwenye mboga, umezidisha sukari kwenye chai”. Mama anavunjwa moyo, hashukuriwi kwa lolote, na zaidi sana atakalipiwa. Ila anang’ang’ana kuwalea watoto wake kwasababu haoni mtu wa kumuachia ili awalee watoto wake. Kuna usemi unaema “Abiria chunga mzigo wako.” Akina mama wamekuwa wakiwachunga watoto wao hata kama wanapitia magumu. Mheshimu Mama!



KWANINI USEME MTOTO MWENYE TABIA MBAYA NI WA MAMA?
Kuna wababa wengine huwa wanadiriki kusema, “Mtoto mwenye tabia nzuri ni wa baba na mtoto mwenye tabia mbaya ni wa mama”. Mama amekuwa ni mtu wa kutupiwa mabaya wakati hayamhusu, amekuwa wa kuonewa sana. Mama ni mzizi katika familia anahitaji heshima yake. Kuna wababa wengine wakiongezewa mshahara utaona wanataka mke mwingine, ukiwauliza utasikia wanasema, “ Sasa hivi ninataka kasichana kamodo modo, huyu wa kwangu ni mnene sana.” Kitu kinachosababisha ni kuwaka tamaa za kimwili. Lakini wacha Mungu wanang’ang’ana na wake zao kwa maana wanajua kuwa kifo ndicho kitakachowatenganisha. Mungu hajaumba mtoto mbaya, wote ni wazuri wala Mungu hajaruhusu kuoa mke wa pili. Ungama sasa.



MKUBALI MKEO KAMA ALIVYO, USIMTUPE.
Mke wako hata akiwa mnene sana, ana matairi au mwembamba kama fimbo mkubali kama alivyo. Wanawake wengi sana wanatelekezwa na waume zao na wanarudishwa kwa wazazi wao. Na hii inatokana na wababa kuwachoka wake zao kwasababu moja au nyingine. Wababa wengi wanasahau yale mema waliofanyiwa na wake zao na wanasahau ule upendo kipindi kile wanachumbiana. Tamaa zao za mwilini zinawafanya kutowatamani wake zao eti kwasababu wamewazoea. Wabab wanatelekeza familia zao na kuwaachia wake zao au bibi na babu. Utakuta babu ameachiwa wajuu sita na vitukuu vya kutosha kwasababu walezi wao wametelekezana. Hii ni tabia mbaya na haipaswi kuigwa na watu.



WAMAMA NDIO KILA KITU CHINI YA JUAHILI; TUWAJALI
Tunapaswa kuwaheshimu wamama kwasababu wao ndio walioleta madaktari, wanasheria, walimu, wafanyabiashara, wakulima, wasomi n.k na wamama hawa wanafanya kazi nzuri; “Hongereni akina mama”. Tukitafakari akina mama wao ndio wapishi wakuu, wamama tukiwaona tunajua leo tunaenda kula “Msosi” na kila mtu anafurahia kumuoa mama jikoni akikorofisha chakula. Wamama wamekuwa wakipika chakula tangia wakiwa wasichana mpaka wameolewa na wengine ni wazee bado wapishi wa chakula. Mgeni akija usiku wao wanaamka kwaajili ya kuwapikia wageni. Kwahiyo mama ni kila kitu chini ya jua hili.



INASIKITISHA KUONA UNAMTESA MAMA YAKO AU MKE WAKO
Wamama wengi wamekuwa wakiteswa na wababa kwa njia moja au nyingine. Mungu atuhurumie akina mama. Wamama wengi wamekosa kibali kwa familia yao na kudharirishwa kwa kufanyiwa kazi nzito na kupewa majukumu mengi kuliko ya baba. Watu bila kutambua jinsi mama alivyohangaika kuwalea, wamekuwa ni watu kama wanyama kwa mama zao. Kama mtumishi wa Mungu, ninasema, “Mungu akupe kibali kwa mume wako, kwa wakwe zako, kwa watoto wako, kwa mawifi zako kwa jina la Yesu Kristo. Ninakataa Roho ya kukataliwa, ninaing’oa kwako kwa jina la Yesu. Mungu akupe kupendwa, kuishi na mume wako mpaka uzeeni, kwa jina la Yesu Kristo. Kila kilichonewa na wabaya wako, nakifunga kwa Jina la Yesu Kristo. Nenda ukang’are mama na ukafurahie maisha yako


WAMAMA WANAPITIA MAGUMU MENGI. NI JUKUMU LETU KUWAJALI
Mara nyingi wamama wamekuwa wakipitia changamoto nyingi sana kuhakikisha watoto wao wanakuwa na maisha bora. Wamama wanaumwa magonjwa ya kila aina baada ya kuwazaa watoto wao. Unajua wanawake wakishazaa wanaanza kupata maumivu ya magoti, mgongo, miguu, nyonga, nyuso zao. Na wakienda hospitalini kufanya oparesheni ya magonjwa hayo ni zaidi ya milioni 10, na utakuta mama hana pesa hiyo kwaajili ya oparesheni hiyo. Unatakiwa kuwaheshimu wazazi wako, na sio kuwaheshimu kwa kusema, “Shikamoo mama” bali uwaheshimu kwa kuwatumia vitu vizuri vinavyoeleweka machoni pa mama yako na watu. Mama yako anapoumwa mpeleke kwenye hospitali nzuri na utapa Baraka
Askofu Dunstan Maboya (kulia) na Mch. Stanley Nnko















































































































Comments