13.05.2018: MCH. PRSCA CHARLES AKISHIRIKIANA NA PRASE & WORSHIP TEMA WALIVYMTUKUZA MUNGU SIKU YA JUMAPILI YA MOTHER'S DAY

//ZABURI 66:1 Mpigieni Mungu kelele za shangwe, nchi yote, imbeni utukufu wa jina lake, tukuzeni sifa zake. Mwambieni Mungu, matendo yako yatisha kama nini!.....//

Hivi ndivyo waumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" walivyomuabudu Mungu na kumuimbia nyimbo za sifa. Katika ibada hii ya UKOMBOZI WA MWANAMKE iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 13.05.2018 watu walimpigia Mungu kelele za shangwe kutokana na kile ambacho Mungu amekuwa akifanya katika maisha yao. Kelele hizo zilikuwa kwaajili ya kumsifu Mungu na kumrudishia Utukufu kwa matendo makuu anayofanya katika maisha ya watu kila kuitwapo leo. Watu walizitukuza sifa za Mungu na kuimba utukufu wake kwa jina lake katika ibada ya UKOMBOZI WA MWANAMKE. Na hii inatokana na matendo yake yanayotisha kama nini katika maisha ya watu.

Kupitia ibada hii ya sifa ambayo iliongozwa na Mch. Prisca Charles akishirikiana na Praise & Worship Team ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" watu wengi walioneka kuguswa na uimbaji huo na pia kuhisi nguvu za Mungu katika miili yao. Nyimbo zilifanyika baraka na faraja kwa walio wengi kutokana na ule ujumbe wa Mungu uliokuwa ukiimbwa kupitia kikundi hicho cha Kusifu na Kuabudu (Praise & Worship Team).

Tunapenda kukushukuru wewe uliyefika katika ibada hii ya Maombi ya UKOMBOZI WA MWANAMKE iliyofanyika siku ya Jumapili ya MOTHER'S DAY. Ni maombi yetu miezi hii iliyobaki ya kumaliza mwaka, Mungu akakupe mke wako/mume wako, kazi yako, biashara yako, maono mapya, wateja wapya, afya njema, ndoa yenye amani na furaha, marafiki wapya wenye mawazo ya kukusaidia kusonga mbele, akili katika masomo yako, watoto wenye afya njema na akili ya ajabu. Mungu akuepushe na mikosi, balaa, nuksi, magonjwa, ndoto mbaya, marafiki wabaya, umaskini, ulemavu wowote ule, mapepo, majini, nguvu za giza, ajali, kutopandishwa mshahara au cheo, kukata tamaa, roho ya kujiua na mambo mabaya kama hayo.

Mungu akupe hamu ya kusoma Neno lake, kwenda kanisani, kuhudhuria ibada za katikati ya wiki, kutamani kutenda yaliyo mema mbele za Mungu na mbele za wanadamu, kuachana na maovu, kuwatii watumishi wa Mungu, kuliishi Neno la Mungu unalosoma katika Biblia yako, kutangaza Injili kupitia huduma yako au karama yako kwa bidiii.

Nenda ukang'are na kuchanua kwa miezi iliyobaki ya kumaliza mwaka 2018. Ukafanikiwe kwa kila jambo, ukafanyika baraka na kwa wengine, ukafanyike msaada kwa wenye uhitaji, ukafanyike asali mbele za watu, ukaheshimike kwa jina la Yesu Kristo.

Yawezekana ulikosa ibada ya Jumapili hii, basi tunakualika katika ibada ya Jumapili ijao ambayo itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Tunakuomba sana kuja na mtu mmoja katika nyumba ya BWANA. Utakapokuja na huyo Mtu naamini Mungu hatakuacha bure, ni lazima atafanya kitu katika maisha yako

Mch. Prisca Charles








































Comments