13.05.2018: HAPPY KWAYA NA JOYBRINGER KWAYA ZAFANYA TUKI LA KUMTUKUZA MUNGU SIKU YA MOTHER'S DAY

//ZABURI 81:1-2: Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha, Mshangilieni Mungu wa Yakobo. Pazeni zaburi, pigeni matari, kinubi chenye sauti nzuri, na kinada,//

Napenda kuwashukuru sana watumishi wa Mungu hawa ambao ni Happy Kwaya na Joybringers Kwaya za Mlima wa Moto Mikocheni "B" , siku ya Jumapili zilifanyika baraka sana katika ibada ya Maombi ya UKOMBOZI WA MWANAMKE iliyofanyika Jumapili ya MOTHER'S DAY Mei.13.2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Waimbaji hawa waligusa mioyo ya watu kutokana na nyimbo zao zenye upako kutoka kwa Mungu. Ujumbe uliokuwa ukiimbwa ulikuwa ni mzito sana wenye kuelimisha, kuadibisha, kufundisha na kuinua imani za watu. Hakika Mungu ni mwema sana kupitia wanakwaya hawa. Nyimbo zao zimejaa mafundisho tosha sana kwa kila mtu aliyebahatika kusikiliza nyimbo zao.

Tuna kila sababu ya kuwashukuru kwa uimbaji wao, kwani kupitia nyimbo zao kuna watu wamepata faraja, wameondolewa usongo wa mawazo, wameburudika, wamebarikiwa na wameweza kuwa karibu na Mungu.

Ni ombi letu ya kuwa unaposikia nyimbo hizi kanisani au katika vyombo mbalimbali, unapaswa kusikiliza kwa makini na kutafakari kile kinachoimbwa na kukifanyia kazi. Usiwe ni mtu wa kusikiliza tu nyimbo bila ya kuyafanyia kazi yale yanayoimbwa. Vile vinavyoimbwa ni ujumbe kutoka kwa Mungu na pia nyimbo zingine ni kwaajili ya kumrudishia Mungu utukufu na kumsifu.

Tuzidi kuwaombea waimbaji hawa pamoja na walimu wao ili wazidi kusikiliza sauti ya Mungu na kuweza kutunga nyimbo zenye mguso wa tofauti katika maisha yetu pamoja na familia zetu..

Yawezekana ulikosa ibada ya Jumapili na unatakamni kushiriki ibada ya Jumapili hii, basi ibada zetu zinaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Tunakuomba sana kuja na rafiki yako au ndugu yako ili naye aweze kuondokana na upako kutoka kwa waimbaji hawa na watumishi wa Mungu wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Mungu anakupenda na dio maana amekupata hata hii nafasi ya kusoma ujumbe hii. Tunakuomba uzidi kumtumikia Mungu na kushiriki ibada zetu bila kukata tamaa. Mungu akubariki sana.

Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3
1 post ·



Joybringer's Kwaya



Happy Kwaya












Comments