06.05.2018: HIVI NDIVYO MAOMBI YA KUKOMESHA UTASA NA KUKARIBISHA MAONGEZEKO YALIYOFANYIKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Hivi ndivyo watu wa Mungu walivyofanya maombi ya KUKOMESHA UTASA NA KUKARIBISHA MAONGEZEKO katika maisha yao siku ya Jumapili 06.05.2018. Maombi haya yalifanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" yakiongozwa na Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare akishirikiana na wachungaji wa kanisa hilo. 

Lengo kubwa lilikuwa ni kukomesha Utasa katika kazi za watu, familia za watu, ndoa za watu, mali za watu, afya za watu, biashara za watu, utasa wa kuzaa, utasa wa kutoshika mimba, utasa wa kupata watoto, kupata promosheni, kupata kibali, kupata safari za nje, kupata marafiki wema, kupata mawazo mapya yenye manufaa na mambo mengine kama hayo. Pia watu waliweza kumuomba Mungu ili afungue milango ya mafanikio katika biashara za watu, mahusiano ya watu, ndoa za watu, familia za watu, kazi za watu, biashara za watu, uzao wa matumbo ya watu, na mengine kama hayo.

Wakati wa maombi kanisa liligubikwa na uwepo wa Mungu ambapo kila mmoja aliweza kupeleka maombi yake ya binafsi kwa Mungu. Baadhi ya watu walionekana kunena kwa lugha na wengine kujazwa Roho Mtakatifu. Ibada hii ilitawaliwa na uwepo wa Mungu na nguvu za Mungu. 

Hakika Mungu wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" amekuwa akionekana na akifanya mambo makuu kila kuitwapo leo hasa kwa wale waaminio, watendao mema na wanaochukua maovu na dhambi. Tumeshuhudia MUngu akiwatendea watu miujiza bila ya ubaguzi kwani Mungu wetu ni MUngu wa haki na asiye na upendeleo.

Unatakiwa kutambua kuwa katika maombi kuna NGUVU ya ajabu sana kutoka kwa Mungu. Unapofanya maombi unasababisha Mungu kufungua milango yako ya mafanikio, unapomuomba Mungu unasababisha Mungu kuwa karibu na wewe wakati huo ili kukusikiliza na kutimiza ndoto zako. Kwahiyo unapoomba unapaswa kumaniisha kwa kile unachoomba, unapaswa kuamini kwa kile ulichomuomba Mungu wetu, unatakiwa kumkumbusha Mungu ili akusaidie kukipata kile ulichokiomba kwa wakati wake, unatakiwa kuwa mvumilivu na jasiri unapofanya maombi. Kuna watu au maadui ambao hawatamani kabisa kukuona unaomba kwani unawaharibia ratiba zao, kwahiyo unapoomba unatakiwa kujipanga na kusimama imara KIIMANI. Usifanya maombi kama haya kwa mazoea. Fanya maombi kwa kumaanisha na utaona mkono wa BWANA katika maisha yako.

Wapo walioomba kwa kumaanisha na sasa wanafurahia matendo makuu ya Mungu. Kwahiyo jiunganishe na wana Mlima wa Moto Mikocheni "B" kkatika Jumapili hii ambayo itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana


Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare 



Mch. Prisca Charles








































































Comments