06.05.2018: DADA MMOJA BAADA YA MIAKA 10 BILA KUPATA MTOTO, MUNGU ASIKIA AOMBI YAKE NA SASA ANA MTOTO

Katika ibada ya KUKOMESHA UTASA NA KUPOKEA MAONGEZEKO kutoka kwa Mungu, iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 06.05.2018, muumini wa kanisa hilo aliweza kumshukuru Mungu kwa kupata mtoto baada ya kilio cha muda wa miaka 10 bila mtoto. Alimshukuru sana Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare na watumishi wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ambao walikuwa wakikesha wakimuombea, na leo Mungu amesikia kilio chake cha mika kumi na kufutwa machozi ya huzuni. Yawezekana unatamani mtoto kwa muda mrefu lakini imeshindikana kupata mtoto unayemhitaji na umekosa amani katika ndoa yako, familia yako na marafiki zako eti huzai. Kila mtu anakusema vibaya kwasababu huna mtoto na umri umekwenda, Umetungiwa majina mabaya na kudharauliwa. lakini leo nataka nikuambie kuwa yupo Mungu anayewapa watu watoto, yupo Mungu anayetenda miujiza kwa kila mtu anayemwamini na kumtumikia kwa uaminifu. Unachotakiwa ni kuwa karibu na huyu Mungu kwa kutenda yale anayokuagiza kupitia kitabu chake kitakatifu yaani Biblia, kusikiliza na kuyatii maagizo na masomo wanayokufundisha watumishi wa Mungu, kuachana na dhambi na kutenda yaliomema machoni pa Mungu na machoni pa watu. Ukiyafanya hayo utaona neema ya Mungu katika tumbo lako. Yawezekana kuna watu wameona udhaifu wako wa kiimani dhidi ya Mungu wako na wakatumia udhaifu huo kukunenea maneno mabaya ili usipate mtoto. Wametupia majini, mapepo, majini mahaba ili usipate mimba na ndoa yako ivunjike. Nataka kukuhakikishi kuwa ukizidi kumtumumikia Mungu kwa uaminifu, utaona mkono wa Mungu katika uzao wako na katika familia yako. Tunakualika katika ibada ya Jumapili hii hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B" ili ukutane na mkono wa Mungu. Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Kanisa limekuandalia usafiri wa bure wa kufika kanisani kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3







Comments