06.05.2018: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ALIA NA WATU WASIORIDHIKA NA KILE WANACHOPEWA NA MUNGU



Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumapili 06.05.2018 katika ibada ya Maombi ya Kukomesha Utasa na Kupokea ONGEZEKO kutoka kwa Mungu katika maisha yetu iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" aliweza kuhubiri juu ya KUTORIDHIKA na hizi ni baadhi ya maada. Fuatilia sasa a;ichokisema,

UNAWAZA NINI JUU YA BWANA?
Kama wanadamu tumekuwa na mawazo mengi sana juu ya maisha yetu na wengine ni kutokana na changamoto za kimaisha. Inafika kipindi unachanganyikiwa kwasababu huoni msaada wowote kutoka kwa ndugu wala jamaa. Waliokupenda wakati unacho wamekuacha peke yako, hawatamani tena kukuona. BWANA anakutia moyo leo kupitia kitabu cha Nahumu 1:9. Je, Kwenye misukosuko uliyonayo, Unawaza nini juu ya BWANA? Je, unafikiri Mungu amekusahau, hakupendi, amekuacha? Ila BWANA anasema, “Atakomesha kabisa mateso yako na hutayaona tena magonjwa wala shida zako”

NAMTUMIKIA MUNGU KWA UJASIRI MKUBWA KWAKUWA NAJUA ALICHONIFANYIA
Timotheo 1:6-11. “Ninamshukuru Mungu kwa kuniokoa kwasababu nilivyokuwa kwenye dini nilijitahidi lakini nikaona dini haiokoi bali nilipookoka niliona mwanga wa mafanikio katika maisha yangu na mapaka sasa bado ninamtumikia Mungu kwa ujasiri mkubwa bila woga kwasababu ninaye Mungu ndani yangu anayenipa nguvu ya kusonga mbele. Watu mataifa wakiniona wanasema “Yule Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ni mama yake Yesu”, na mimi ninawajubu, “Mbele Kwa Mbele, watajaza wenyewe.”, “mimi ndiye mama wa Yesu,” kwasbabu ni mengi kanitendea katika maisha yangu

USIWE NA ROHO YA KUTORIDHIKA
Ni kweli tunatambuwa kuwa kama Wakristo, tumeokoka, tunakwenda mbinguni, tunaimba pambio, tunamtukuza Mungu lakini unapokaa nyumbani mwa BWANA kuna watu wenye Roho ya kutorithika. Hatukatai kuwa mtu lazima atafute yale makubwa ambayo moyo wake unataka. Lakini usiwe tayari kufanya UHARIBIFU ili kujilinganisha na mtu fulani aliyefanikiwa. Kama vile vidole vilivyo, kuna vidole virefu na vingine vifupi, basi na sisi wanadamu lazima TURIDHIKE kutokana na kile tunachokipata au tunachobarikiwa na Mungu. Ni kweli tunatafuta kwasababu tunataka tuishi kwa raha, lakini tutambue kuwa sisi wenyeji wetu sio duniani ni mbinguni. Tamaa yako isikufanye ukamkufuru Mungu kwa kutoridhika.

FAIDA YA KURIDHIKA NA HALI YAKO
Mtu asiyeridhika huingiwa na roho ya tamaa na wivu dhidi ya mtu aliyeridhika. KURIDHIKA kutakuondolea uchungu, wivu, kujilinganisha, dharau, kutungiwa majina mabaya n.k. Lakini tuliyeokoka lazima tutambue kuwa ni watoto wa Baba mmoja wa mbinguni, tunaelekea mbinguni kwahiyo tunatakiwa sisi sote tuwe na furaha pale furaha inapomuangukia mmoja na wote tuwe na uchungu pale uchungu unapomuangukia mmoja. Kipindi nimeokoka mtu akipatwa na shida anakuwa wazi kumwambie mwenzake. Kanisa la sasa likiwa na watu wenye kuridhika na kumshukuru Mungu kwa kila jambo hakika kanisa hili litakwenda mbinguni. Nisingependa kubeba watu kanisani ambao hawataingia mbinguni. Natamani wote tumuone Mungu

TAMAA NI TUNDA LA KUTORIDHIKA
Mimi kama Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ni dua yangu na maombi yangu ya kuwa kama tulivyo hapa kanisani siku ya mwisho twende tukamlaki Yesu Kristo, na nisimuache hata mtu mmoja eti kwasababu ana dhambi ya kutoridhika. Watu wengi wamefanya dhambi za ajabu kwasbabu ya KUTORIDHIKA. Mtu mmoja asiyeridhika na hali yake alimchukua mjomba wake akampeleka kwa wachuna ngozi ili apate milioni sita (6) kwa njia ya ushirkikina na kumfanyia kafara, hii ni dhambi mbaya sana. Baadhi ya watu wa Mbeya huko Mbozi enzi hizo walikuwa tayari kutoa ngozi za wenzao ili wapate mali. Marko 1:36 Itakusaidia nini mtu apate ulimwengu wote na baadae apoteze nafsi yake asiende mbinguni, itakusaidia nini ukapata milioni sita na baadae usiingie mbinguni!

KUTORIDHIKA KWAKO KUTAKUPELEKA JEHANAMU
Umekuwa ukishiriki ibada, ukiimba, ukisali, ukijinyima anasa zote, ukiabudu, ukitoa zaka lakini mwisho wa siku unakwenda motoni kutokana na dhambi ya KUTORIDHIKA. Mungu anasema, “Zikimbieni tamaa kama hizo za watu wa dunia kwa maana ninyi ni watoto wa Mungu.” Kuna watu wanaua albino, wanakatwa vioungo vyao kutokana na watu kutoridhika na maisha ambayo Mungu amewapa. Kuna siku moja tulienda kwa tajiri mmoja tukamkuta mtoto wa miaka kama 26 yupo sebuleni anachekacheka tu, anaangalia TV hajielewi kumbe amefanyiwa kuwa ndondocha na baba yake ili apate mali, ukimuuliza swali anajibu, “Mimi ni darasa la kwanza.” Sisi ni watoto wa Mungu tunapaswa kuridhika. Maendeleo yetu ni foleni, leo yeye ila kesho wewe.

KUTORIDHIKA KWAKO KUTAKUPELEKA JEHANAMU
Umekuwa ukishiriki ibada, ukiimba, ukisali, ukijinyima anasa zote, ukiabudu, ukitoa zaka lakini mwisho wa siku unakwenda motoni kutokana na dhambi ya KUTORIDHIKA. Mungu anasema, “Zikimbieni tamaa kama hizo za watu wa dunia kwa maana ninyi ni watoto wa Mungu.” Kuna watu wanaua albino, wanakatwa vioungo vyao kutokana na watu kutoridhika na maisha ambayo Mungu amewapa. Kuna siku moja tulienda kwa tajiri mmoja tukamkuta mtoto wa miaka kama 26 yupo sebuleni anachekacheka tu, anaangalia TV hajielewi kumbe amefanyiwa kuwa ndondocha na baba yake ili apate mali, ukimuuliza swali anajibu, “Mimi ni darasa la kwanza.” Sisi ni watoto wa Mungu tunapaswa kuridhika. Maendeleo yetu ni foleni, leo yeye ila kesho wewe.

Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare



























Comments