06.05.2018: BAADHI YA WATU WALIOBATIZWA KATIKA IBADA YA KUKOMESHA UTASA NA KUPOKEA MAONGEZEKO YA BARAKA KUTOKA KWA MUNGU

Baada waongofu wapya kuongozwa sala ya toba, kuombewa na kushiriki ibada ya maombi ya KUKOMESHA UTASA NA KUPOKEA BARAKA ZA MAONGEZEKO KUTOKA KWA MUNGU katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 06.05.2018, waongofu hawa wapya waliweza kubatizwa kwa maji mengi. Tunamshukuru sana Mungu kwa kile alichokifanya kwa waongofu wapya wakati wakibatizwa, tulishuhudia watu wakipokea Roho Mtakatifu, wakipata nguvu mpya kutoka kwa Mungu, wakiwa na furaha ya ajabu ndani ya mioyo yao kwasbabu kuna kitu kilitokea wakati wakibatizwa na watumishi wa MUngu.

Tunapenda kuwapongeza waongofu wapya kwa kuchukua maamuzi ya kumrudia Mungu, kuachana na maisha ya zamani na kufanyika watoto wa Mungu tena. Tunawashukuru sana watu waliohusika kuwahubiria Habari Njema za Mungu na zikaweza kuingia katika fam=hamu zao wakaamua kuokoa na kubatizwa.

Wachungaji, wainjilisti, walimu na wahudumu wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" wakishirikiana na Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare wamefanyika baraka kubwa sana ya kuwatoa hawa waongofu wapya kutoka katika shimo la mateso na kuwaweka nuruni mwa BWANA.

Tunaamini kwaazia sasa maisha yao yatabadilika, kama walikuwa hawana watoto watapata watoto, kama walikuwa hawana kazi watapata kazi, wataolewa na kuoa, watapandishwa vyeo, watapata promosheni makazini mwao, watakuwa na majumba na magari, watabarikiwa, kiwango cha imani kitabadilika, watapata kibali, wataheshimika, watakuwa nguzo katika familia zao, watakuwa watumishi wakubwa wa Mungu, na mambo mengine kama hayo. Mungu hatawaacha waabike kwasababu wamemrudia Yeye muweza wa yote.

Tuzidi kuwaombea hawa waongofu wapya wazidi kumtumikia Mungu, wazidi kusonga mbele kwa kazi ya Mungu, wazidi kuwaokoa na wenzao ili nao waokoke kama walivyofanyiwa wao, wazidi kutenda mema na kuachana na dhambi, anasa za dunia na kila kitu kiovu. Mungu ainue na kuzibariki kazi za mikono yao, familia zao, biashara zao na ndoa zao n.k.

Siku ya Jumatatu na Jumanne waongofu hawa waliendelea na masomo yao ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kila siku saa 10 jioni.

Yawezekana na wewe unatamani kuokoka, unatamani kumtumikia Mungu, unatamani kuwa katika familia ya Mungu, unatamani kubatizwa na kuwa mtoto wa Mungu usiye na doa, kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" linakualika katika ibada ya Jumapili hii kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Siku hiyo kutakuwa na muda maalum kwako wewe kupata nafasi ya kuongozwa sala ya toba na kubatizwa kwa maji mengi. Na siku ya Jumatatu na Jumanne utaingia darasani kwaajili ya kujifunza masomo ya kukulia wokovu.

Muda wako ni sasa wa kurudi kwa Mungu na kumtumikia Mungu ukiwa bado una nguvu. Wapo wengi wanatamani kuokoa lakini wamefungwa na magonjwa, wamefungwa na giza nene la kutambua wema wa Mungu, wamelogwa ili wasione umuhimu wa kuokoka, wamenenewa maneno mabaya kwa waganga ili wazidi kumtumikia shetani maisha yao yote. lakini wewe uliyepata neema ya kusoma ujumbe, nakuomba uchukue hatua sasa ya kuja kanisani ili ubatizwe kwa maji mengi ili siku yako ya kuondoaka hapa duniani uweze kwenda mbinguni na kuonana na Mungu wako.

Kanisa limekuandalia usafiri wa bure wa kufika kanisani kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3
Mch. Asenga















































Comments