15.10.2017: MAOMBI YA KUOMBEA MAJI KWAAJILI YA KUVUNJA NGUVU ZA UGANGA NA UCHAWI

Baada ya maombezi ya Kuvunja Nguvu za Uganga na Uchawi kumalizika siku ya Jumapili 15.10.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kugawa maji kwa wale ambao walisahau kuja na maji ya baharini ili yaombewe na baada ya kuombewa wale wachawi wa baharini na mapepo ya bahari, nguvu za giza majini ya baari yateketezwe kwa jina la Yesu Kristo. Watu wengi sana walikuja na maji yao ya bahari ili yaombewe na ambao hawakuja na maji waligawiwa kanisani.

Wapo watu wengi sana wanateseka na nguvu za giza, wachawi na waganga wamewaloga na mambo yao hayaendi mbele. Kila jambo wanalofanya halifanikiwi, kila wakijitahidi hakuna matunda wanayopata. Kila wakipata fedha matatizo ndani ya nyumba au familia yanajitokeza. Shetani ameteka fahamu zao, akili zao, maarifa yao ili wasifanikiwe. Wengine wamefungwa kamba kama mbuzi, kila wanachofanya kiinaishia urefu wa kamba yao.

Jamani shetani hana huruma, na sisi tunatakiwa kutokuwa na huruma naye. Ni wakati wako wakusimama kidete kwa maombi na kutupa makombola ya kuwaangimiza hawa wachawi na kuwaweka hadharani ili waabike mbele za watu.

Yawezekana ni mmojawapo ya watu wanaopitia mateso katika ndoa yako, familia yako, kazi yako, mifugo yako, huduma yako, biashara yako, malengo yako, mahusiano yako, uchumba wako, uzao wako, mimba yako, unaota ndoto chafu na mbaya, unalishwa vitu vya ajabu usiku. Nataka ni kwambie kuwa Jumapili hii itakuwa ni komesha mateso. Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Njoo na ndugu yako au rafiki yako ukutane na nguvu za Mungu...
Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare











































Comments