15.10.2017: MAMIA YA WATU WAOKOKA KATIKA IBADA YA KUVUNJA NGUVU ZA UCHAWI NA UGANGA ILIYOFANYIKA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Baadhi ya watu waliokoka siku ya Jumapili 15.10.2017 katika ibada ya KUVUNJA NGUVU ZA UGANGA NA UCHAWI iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Watu hawa kabla ya kubatizwa waliongozwa sala ya toba, wakaombewa na baadae kubatizwa kwa maji mengi. Katika zoezi la kuwabatizwa tulishuhudia nguvu za Mungu zikifanya kazi kwa watu hawa. Watu wengi walitokwa na mapepo na roho chafu zilizokuwa zikiwasumbua kwa muda mrefu huku wapiga kelele wakihitaji kuwekwa huru. 

Tunawashukuru watumishi wa Mungu waliweza kufanya maombi ya tofauti sana kwa watu hawa na kuhakikisha mapepo yaliyokuwa yakiwasumbua kwa muda mrefu yakiwatoka na kuwaacha wakiwa huru. Watu hawa waliweza kumpokea Roho Mtakatifuat akayewaiongoza katika maisha yao na huyo ndiye atakayewaongoza pale watakapokumbwa na majribu ya shetani.

Baada ya kubatizwa waliweza kupata vinywaji na watumishi wa Mungu na kutiana moyo. Siku ya Jumatatu na Jumanne ni siku zao maalum za kuanza masomo ya kukulia wokovu ambayo huanza saa 9 alasiri ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Yawezekana unatamani kuokoka na kubatizwa lakini hujui utaanzia wapi, tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 8 mchana. Watumishi wa Mungu watakuongoza sala ya toba, watakuombea, watakubatiza na utafundishwa masomo ya kukulia waokovu ambao umeupata bure.

Baada ya Kubatizwa siku ya Jumapili, siku ya Jumatatu na Jumanne zitakuwa ni siku zako za mafundisho ya kukulia wokovu.

Ndugu yangu okoka sasa na batizwa sasa, itafika kipindi utashindwa hata kupata nafasi ya kuongea na kuhitaji ubatizo. Hujui kitu gani kitakukumba baada ya hapa. Na wewe uliyeokoka na kubatizwa haijaishia hapo, endelea kutenda mema, kusoma Neno la Mungu na kuliishi, kuhudhuria ibada, kuachana na dhambi na mengine kama hayo.

Mungu anakupenda, tukutane kanisani Jumapili hii. UBARIKIWE.
















































































 xxxxx

Comments