15.10.2017: HAPPY KWAYA NA JOYBRINGERS WAFANYIKA BARAKA KATIKA IBADA YA KUVUNJA NGUVU ZA UCHAWI NA UGANGA

Inapendeza kuona kila kuitwa leo unamtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji. Hivi ndivyo ilivyokuwa katika ibada ya Kuvunja Nguvu za Uchawi na Uganga iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 15.10.2017. Happy Kwaya na Joybringers Kwaya za Mlima wa Moto Mikocheni "B" zilimtukuza Mungu kwa kuimba na kucheza. Ilikuwa ni siku ya furaha na shangwe katika nyumba ya BWANA. Waimbaji hawa wamefanyika nguzo ya kanisa kwa uimbaji wao, watu wengi sana wanabarikiwa na kupokea miujiza yao kupitia watumishi wa Mungu hawa.

Unajua Mungu amegawa vipawa kwa kila mtu, na kila kipawa kina umuhimu kwa maisha ya mtu mwingine. Kupitia uimbaji wapo watu wanafarijika, wanaondolewa usongo wa mawazo, wanaburudika, wanabarikiwa, wanajifunza kupitia ujumbe unaoimbwa kutoka kwa watumishi wa Mungu.

Tuna kila sababu ya kuwaombea watumishi hawa ili wasonge mbele. Kazi yao ni njema mbele za Mungu na mbele za wanadamu. Waombee ili wazidi kufanikiwa kimwili na kiroho ili nasi tuzidi kubarikiwa kutoka kwao. Unapofanya maombi yako usisahau kuwaombewa waimbaji hawa ili wababrikiwe zaidi ya hapo walipobarikiwa.

Mungu ni mwamanifu, atasikia maombi yako na atayafanyia kazi kwa uaminifu.

Tukukaribishe Jumapili hii katika ibada iliyojaa nguvu za Mungu itakayoanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Njoo na rafiki au ndugu yako ili naye apokee baraka za Mungu. Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Baada ya ibada utarudishwa kituoni bila malipo
















Comments