15.10.2017: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ALIVYOMSIFU MUNGU NA WAUMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" KATIKA IBADA YA KUVUNJA NGUVU ZA UCHAWI NA UGANGA

Kanisa lilijawa na furaha na upendo katika kipindi cha kumsifu Mungu kilichoongozwa na Mch. Prisca Charles siku ya Jumapili 15.10.2017 katika ibada ya KUVUNJA NGUVU ZA UCHAWI NA UGANGA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliungana na waumini wa kanisa hilo kwaajili ya kumsifu Mungu kwa kucheza na kuimba huku wakimshukuru ungu kwa matendo makuu aliyoyafanya katika maisha yao tangia Januari hadi mwezi huu tulionao.

Hii ilikuwa ni ibada ya tofauti sana, kulikuwa na uwepo wa Mungu ndani ya kanisa, nguvu za Mungu na pia sura za furaha kwa kila aliyetambua umuhimu wa kumsifu Mungu... Hakika watu walimsifu Mungu.....kwa roho wa kweli...

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa yale anayoyafanya katika kanisa lake hili la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Kupitia sifa watu wanapokea miujiza yao...

Wapo watu wanafunguliwa, wanaponywa, wanapokea baraka za Mungu, wanafarijiwa, wanaondolewa usongo wa mawazo, wanainuliwa, wanavutiwa kuokoka, wanainuliwa imani zao kupitia nyimbo za sifa. Kwahiyo huduma hii ya kumsifu Mungu ni moja ya nguzo kubwa sana katika kusaidia watu kuwa na ile hofu ya Mungu.

Mungu wetu ni Mungu wa sifa, kwahiyo watu wake wanapomsifu kwa kuimba na kucheza basi Mungu wetu wa mbingunu anafurahi na anakuwa katikati yao. Kwahiyo unapokuwa kanisani katika kipindi cha kusifu na kuabudu, imba kwa kumaanisha na sio kuimba kwa kufuata mkumbo. Ukiimba kwa kufuata mkumbo hutaona uwepo wa Mungu na hataona nguvu za Mungu katika maisha yako. Imba ukimaanisha na usiangalie watu wengine, cheza kwa kumaniisha na usiangalie watu wengine, usiimbe kwa kutaka sifa au uonekane unaimba bali imba ukijua unamuimbia Mungu wako. Umekuja kanisani peke yako, kwahiyo fanya yako kwa kumaniisha na utaona upendo wa Mungu kwako.

Tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Kwa wale wanaohitaji kuokoka na kubatizwa wataoongozwa sala ya toba, wataombewa na kubatizwa. Na wale wenye mahitaji ya kuombewa wataombewa na watumishi wa Mungu baada ya ibada kumalizika. Pia kutakuwa na maombi ya watu wote kabla ya ibada kuisha. Mungu na akubariki sana.







































Comments