15.10.2017: BAADHI YA WATU WALIOKOKA KATIKA IBADA YA KUVUNJA NGUVU ZA UGANGA NA UCHAWI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

15.10.2017: MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B": WALIOKOKA
Mch. Elizabeth Lucas wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 15.10.2017 katika ibada ya KUVUNJA NGUVU ZA UGANGA NA UCHAWI aliweza kuwaongoza sala ya toba watu waliokoka siku hiyo. Baada ya kuongozwa sana ya toba, waliombewa na kubatizwa kwa maji mengi. Siku ya Jumatatu na Jumanne ni siku zao za kujifunza masomo ya kukulia wokovu yanayoanza saa 9 alasiri ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Kipindi wanaombewa baadhi yao walitokwa na nguvu za giza, mapepo na majini. Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa matendo makuu anayoyafanya katika kanisa la Mlima wa Moto Mikcheni "B". Watu wengi sana wanaokoka na kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao, watu wanafunguliwa kutoka katika vifungo vya shetani na kuwekwa huru.

Wapo watu wengi sana wamekuwa wakifika katika kanisa hili wakiwa hawajaokoka wakiwa na mizigo ya mizto ya kutooa/kuolewa, wkutopata kazi, wasiopandishwa mishahara yao, wasiozaa, wenye shida ya mimba kuporomokoa, wanaologwa na wachawi, wasiotimiza malengo yao, waliolaaniwa na ndugu zao, wenye magonjwa mbalimbali, waliokata tamaa n.k lakini baada ya kuokoa na kumpokea Yesu Kristo kuwa namba moja katika maisha yao, mambo yakaanza kufunguka na sasa wanafurahia matendo makuu ya Mungu.

Ukiwa ni mtu wa IMANI na unamtegemea MUNGu kwa kila jambo na kuyatimiza yale anayokuagiza katika Biblia yake, hakuna litakalokushida. Wapo watu wengi sana walioamua kuendesha maisha yao kwa kumtanguliza Mungu mbele, na maisha yao yamekuwa bora na tunatumaini siku ya mwisho watamuona Mungu. Ni

Wewe ambaye hujaokoka tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Kutakuwa na muda maalum kwaajili yako. watumishi wa MUngu watakuongoza sala ya toa, watakuombewa, utabatizwa na utapa muda mzuri wa kuongea na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Siku ya Jumatatu na Jumanne utaanza masomo ya kukulia wokovu.

Mch. Elizabeth Lucas






































Comments