08.10.2017: MH. BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AWAOMBEA WAMAMA WAJAWAZITO KATIKA IBADA YA KUVUNJA NIRA

Katika ibada ya KUVUNJA NIRA iliyofanyika Jumapili 08.10.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B, Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kuwaombea akina mama wote wenye ujauzito ili Mungu azidi kuwalinda kwa kipindi chote mpaka watakapojifungua.

Unajua katika dunia hii, kuna watu wabaya ambao mioyo yao ni kuona watu wanapatwa na mabaya. Wapo watu wengine hawatamani kuona wenzao wanapata watoto. Lengo la watu hawa ni kuharibu mimba za watu kwa kwenda kwa waganga au kuwatamkia maneno mabaya ili watoto watakapozaliwa wawe mazezeta au wasio na muelekeo wa maisha. Kwa kuona hilo Mh. Bishop dr. Gertrude Rwakatare na kanisa zima walitenga muda maalum kwaajili ya kuwaombea na kuomba damu ya Yesu iwafunike.

Wakati wa maombezi baadhi yao mapepo yalianza kupiga kelele kutoka na nguvu za Mungu na moto ulao ulivyokuwa ukiwaunguza. Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwasababu akina mama hawa walifunguliwa kutoka nira zilizowafunga kwa muda mrefu.

Wewe mama mjauzito na umekuwa ukipitia changamoto mbalimbali katika kipindi chako cha ujauzito, tunakukaribisha Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili saa 3 asubuhi au saa 8 mchana au siku za katikati ya wiki saa 9 mchana ili ufanyiwe maombi, na Mungu aingilie katika katika hali yako ya ujauzito. Mungu akubariki sana.






















Comments