08.10.2017: MAOMBI YA KUWAOMBEWA WAMAMA NA WADADA WANAOHITAJI WATOTO YAFANYIKA KATIKA IBADA YA KUVUNJA NIRA

Maombi maalum ya kuwaombea wamama na wadada wenye uhitaji wa watoto yalifanyika siku ya Jumapili 08.10.2017 katika ibada ya KUVUNJA NIRA ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Watu wengi sana walijitokeza katika madhabahu ya BWANA baada ya Mch. Noah Lukumay kuwaita ili wafanyiwe maombi

Unajua, kuna watu wengi sana wanahitaji watoto lakini imekuwa ngumu sana kuwapata, baadhi yao mimba zinaharibika, hawashiki mimba na wengine watoto wanafia matumboni. Baadhi yao wanabahatika kuzaa lakini baada ya muda fulani mtoto anafariki. Watu kama hawa wamekubwa na roho chafu iliyotumwa kutoka kwa maadui zao.


Siku ya Jumapili Mungu aliweza kuwakumbuka na kutuma majeshi yake kupitia mtumishi wake Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ili kuangamiza na kusamabaratisha roho mbaya zinazowakumba akina mama wengine kupata mimba au kuzaa watoto. 


Unatakiwa kujua kuwa sio kila mtu anatamani kuona mtu mwingine anafanikiwa na ndio maana watu wamekuwa wakilogana na kufanyiana ushirikina ili kuharibiana. Watu wabaya wanatamani kukuona ukiteseka na kunung'unika kila wakati, hawataki kukuona una furaha, unamaendeleo katika maisha yako. baadhi ya wamama wanakumbwa na hili tatiozo kutoka kuambukizwa kutoka kwa wazazi wao au mababu zao (hasa wale ambao hawajamjua Yesu Kristo)

Baadhi ya watu wamepata madhara makubwa sana katika ndoa zao kwa tatizo la kutopata watoto au kushika mimba. Ndoa nyingi zimevunjika na zingine kumekuwa na migogoro isiyoisha.

Mh. Bishop Dr. Gertrude rwakatare baada ya kusikia kilio cha wamama na wadada wanaopitia changamoto ya kupata mimba au kupata watoto, aliamua kuwaombea, kuvunja nguvu za giza na roho chafu ili watu hawa wakapate watoto na kushika mimba.

Pengine na wewe unapitia changamoto hii ya kutoshika mimba au kutozaa na umehangaika bila ya majibu, tunakusihi njoo katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana tukuombee. Ndugu yangu maombi yana nguvu na huleta majibu kama utaomba kwa imani na kuwa mvumilivu.

Mungu akubariki sana.

Mch. Noah Lukumay








Comments