08.10.2017: JONATHAN KIBONA NA MKE WAKE HAPPINES WAKIMSHUKURU MUNGU KUWAFANIKISHA KUFUNGA NDOA YAO SALAMA

Jonathan Kibona na mke wake Happines siku Jumapili 08.10.2017 katika ibada ya KUVUNJA NIRA waliweza kumshukuru Mungu kwa kuwalinda na kuwafanikisha katika ndoa yao iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".  Walimshukuru Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa malezi yake ya kiroho na upendo aliokuwa nao tangia akiwa mtoto na sasa ameweza kuoa. Waliwashukuru wazazi wao,  wazee wa kanisa, vijana, wainjilisti, wachungaji, na bila kumsahau Mch. Noah Lukumay ambaye kwa kipindi chote amekuwa karibu nao na kuwashauri ple walipohitaji msaada wa kimawazo
























Comments