08.10.2017: BWANA HARUSI MTARAJIWA AMVISHA PETE YA UCHUMBA MCHUMBA WAKE KATIKA IBADA YA KUVUNJA NIRA

Wanandoa watarajiwa hawa siku ya Jumapili 08.10.2017 katika ibada ya KUVUNJA NIRA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", Bwana harusi mtarajiwa aliweza kumvisha mchumba wake pete ya uchumba madhabahuni. Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa hawa wanandoa watarajiwa kwa maamuzi yao ya busara na hekima walioyafanya, yamefanyika baraka katika kanisani na familia yake. 

Mch. Noah Lukumay aliweza kuwaombea na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliwatamkia maneno ya baraka.

Yawezekana kilio chako ni kupata mume au mke, umehangaika bila mafanikio na unaona umri wako unaenda. Tunakukaribisha katika madhabahu iletayo majibu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" upokee muujiza wako wa mume/mke. Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Hata hawa ndugu zetu waliamua kuthibitisha kanisa kuwa ni wachumba, siku za nyuma walikuwa na kilio kama chako cha kutaka kuoa/kuolewa, lakini walipokanyaga katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" wameweza kupokea muujiza wao kutoka kwa Mungu..

Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare amekuwa akiwatamkia watu maneno ya baraka na watu wamekuwa wakipokea wachumba wao, wake zao na Mungu amekuwa akijibu maombi yao kwa wakati wake. Yawezekana Jumapili hii ikawa ni zamu yako. Njoo kanisani ukiwa na IMANI ya kupokea muujiza wako.






















Comments