08.10.2017: BAADHI YA MAMIA YA WATU WALIOKOKA KATIKA IBADA YA KUVUNJA NIRA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Hawa ni baadhi ya watu waliokoka katika ibada ya KUVUNJA NIRA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" iliyoongozwa na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Mch. Elizabeth Lucas na Mch. Francis Machichi waliwaongoza sala ya toba na kuwaombea. Wakati wakiombewa tulishuhudia baadhi yao wakitokwa na mapepo na majini huku wakupiga kelele. Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa yale aliyoyafanya kwa watu wake.

Baada ya kuongozwa sala ya toba na kufanyiwa maombezi walipelekwa mahali maalum kwaajili ya kubatizwa kwa maji mengi. Siku ya Jumatatu na Jumanne wataanza masomo yao ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 9 alasiri.

Yawezekana hujaokoka na pengine umekuwa ukipitia changamoto mbalimbali, umekuwa ni mtu wa kulia kutoka na mapito unayopitia, lakini leo nataka nikupe habari njema kuwa yule Yesu mtenda miujiza anakuita njoo uokoke. Utakapookoka tu utashangaa mambo yako yakikunyooke kimwili na kiroho.

Chukua hatua na maamuzi thabiti ya kuja kwa Yesu ili upumzishwe na mizigo ya mateso unayopitia. Maadui zako wamekutumikisha kwa muda mrefu, sasa yatosha kwani yupo Mungu ambaye ni mtetezi wa maisha yako.

Wewe unahitaji kuokoka usikose ibada ya Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana kutakuwa na watumishi wa Mungu watakaokuongoza sala ya toba, watakuombea na utabatizwa kwa maji mengi.
Mch. Elizabeth Lucas












































Comments