01.10.2017: WAMAMA WENYE UVIMBE WAFANYIWA MAOMBI MAALUM KATIKA KONGAMANO LA WANAWAKE NA UCHUMI (WOCA)

Katika hitimisho la Kongamano la Wanawake na Uchumi la Kukomesha Kilio Cha Mwanamke lililofanyika siku ya Jumapili 01.10.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Bishop Dunstan Maboya na wachungaji waliweza kufanya maombi maalum ya uponyaji kwa watu wenye uvimbe na wenye magonjwa mbalimbali. Baadhi yao walipokea uponyaji hapo kwa hapo na wakashuhudia mbele ya madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" jinsi Mungu alivyowaponya.
Kongamano hili liliandaliwa na Chama Cha Women For Christ Alliance (WOCA) cha Mlima wa Moto Mikocheni "B"kwa muda wa siku 8.
Wewe ambaye ulikosa kuhuduria kongamano hili unaweza kupata mahubiri kutoka YOUTUBE.
Tunakualika katika ibada ya Jumapili hii itakayoanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kunzia kituo cha mabsi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola.














Comments