01.10.2017: BAADHI YA WATU WALIOKOKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" KWENYE KONGAMANO LA WANAWAKE NA UCHUMI

Siku ya Jumapili 01.10.2017 katika hitimisho la kongamano la wanawake na uchumi la kukomesha kilio cha mwanamke baadhi ya watu waliweza kuokoka na kubatizwa kwa maji mengi. Katika zoezi la kubatizwa tulishuhudia watu wakitokwa na mapepo, majini na nguvu za giza zilizokuwa zikiwasumbua kwa kipindi kirefu. Tunamshukuru Mungu kwa wema wake na huruma zake juu ya watu hawa ambao waliamua kufanya maamuzi ya busara ya kumpokea Yesu Kristo kuwa BWANA na Mwokozi wa maisha yao.

Baada ya kubatizwa, siku ya Jumatatu na Jumanne walianza masomo yao ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Kongamano hili liliandaliwa na chama cha Women For Christ Alliance (WOCA) cha kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".




















































































Comments