01.10.2017: BAADA YA KUHITIMISHWA KWA KONGAMANO LA WANAWAKE NA UCHUMI - WOCA PICHA ZA KUMBUKUMBU ZAPIGWA KANISANI

Baada ya kuhitimisha kongamano la wanawake na uchumi la kukomesha kilio cha mwanamke siku ya Jumapili 01.10.2017 baadhi ya wazee wa kanisani na waumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" waliweza kupiga picha ya pamoja ya kumbukumbu.

Kongamano hili lilianza tarehe 24.09.2019 na kuhitimishwa tarehe 01.10.2017. Lengo kubwa la kongamano hili lilikuwa ni kumkwamua mwanamke katika hali ya umaskini wa kimwili na kiroho. Walimu wa maswala ya UCHUMI na watumishi wa Mungu mbalimbali waliweza kutoa elimu kwa waumini wa kanisa hilo na wageni waliofika kujifunza.

Kongamano hili liliandaliwa bure kabisa na Chama Cha Women For Christ Alliance (WOCA) - Mithali 31:29 na kuwaalika walimu wa mambo ya ujasiriamali kama vile Bw. Mashauri, Mch. Dkt. Peter Mitimingi, Mary Ngowi, Esther Mukasa, pia kulikuwa na watumishi wa ungu kama vile Bishop Dunstan Maboya na mwenyeji Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.





























Comments